Winga wa Paris Saint-Germain (PSG) na timu ya Taifa ya Ufaransa, Ousmane Dembélé, ametangazwa mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kiume wa FIFA kwa mwaka 2025, baada ya msimu bora uliompa heshima hiyo ya juu duniani.
Kocha wa PSG, Luis Enrique, naye ameendeleza mafanikio ya klabu hiyo kwa kutwaa Tuzo ya Kocha Bora wa Kiume wa FIFA 2025, akitambuliwa kwa mchango wake mkubwa katika mafanikio ya timu hiyo ya Ufaransa.
Katika tuzo za walinda mlango, Gianluigi Donnarumma, ambaye kwa sasa anachezea Manchester City na aliwahi kuitumikia PSG msimu uliopita, ameshinda Tuzo ya Golikipa Bora wa Kiume wa FIFA 2025.
PSG pia imeonyesha ubabe wake kimataifa baada ya kuwa na wachezaji watano walioteuliwa kuingia kwenye Kikosi Bora cha FIFA cha mwaka 2025, wakiwemo Achraf Hakimi, Willian Pacho, Nuno Mendes, Vitinha na Ousmane Dembélé.
Wachezaji wengine waliounda kikosi hicho bora ni Gianluigi Donnarumma (Manchester City), Virgil van Dijk (Liverpool), Cole Palmer (Chelsea), Jude Bellingham (Real Madrid) pamoja na Pedri na Lamine Yamal wa Barcelona.