AFCON 2025: Aubameyang Aikosa Mechi ya Kwanza, Anaweza Kurudi Dhidi ya Mozambique

Shirikisho la Soka la Gabon 🇬🇦 limethibitisha kuwa mshambuliaji wao nyota, Pierre-Emerick Aubameyang (36), hatawepo kwenye mchezo wa ufunguzi wa AFCON 2025 dhidi ya Cameroon 🇨🇲 utakaochezwa Disemba 24, kutokana na majeraha yanayomsumbua.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Aubameyang anaweza kurejea uwanjani Disemba 28 wakati Gabon itakapokutana na Mozambique 🇲🇿, endapo hali yake ya afya itaendelea kuimarika.

Kukosekana kwake dhidi ya Cameroon ni pigo kwa Gabon, ikizingatiwa mchango wake mkubwa katika safu ya ushambuliaji na uzoefu wake kwenye mashindano makubwa ya kimataifa.