Kocha Yanga SC aomba kazi Simba SC

BAADA ya Dimitar Pantev kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Simba SC inatajwa kuwa kuna maombi ya makocha mbalimbali wametuma CV kukinoa kikosi hicho.

Kwa sasa timu hiyo ipo chini ya Seleman Matola ambaye mchezo uliopita alishuhudia kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Azam FC wakiwa Uwanja wa Mkapa.

Hicho ni kipigo cha kwanza Simba SC msimu wa 2025/26 kwenye ligi ikiwa ni mechi za mwanzo mnyama anapoteza pointi tatu akiwa nyumbani.

Taarifa zinaeleza kuwa miongoni mwa makocha ambao wametuma CV ili kupata nafasi kukinoa kikosi hicho ni pamoja na makocha ambao waliwahi kufundisha Yanga SC kwa nyakati tofauti.

Luc Eymael kocha mwenye maneno mengi huyu anatajwa kutuma CV kwa uongozi wa Simba SC ili kurithi mikoba ya Pantev.

Mbali na huyo jina la Romain Folz kocha wa minuno ambaye aliifunga Simba SC alipokuwa akikifundisha kikosi cha Yanga SC kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii anatajwa kutuma CV.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.