Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Miguel Gamondi, amesema wachezaji wake wanaonyesha bidii kubwa mazoezini na kwamba morali ipo juu kuelekea mashindano ya AFCON 2025.
Gamondi ameyasema hayo leo Desemba 15, baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu, akisisitiza kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na wachezaji wanaelewa majukumu yao ndani ya uwanja.
Kocha huyo amewataka Watanzania kuwa na imani na timu, akieleza kuwa mashabiki wanapaswa kutegemea kuona soka zuri, lenye nidhamu, kasi na ushindani mkubwa, kulingana na mpango wa kiufundi anaouandaa mazoezini.
“Wachezaji wanajituma kwa kiwango kikubwa, kuna mshikamano mzuri na ari ya ushindi ipo juu. Tunajenga timu itakayocheza mpira wa kuvutia na wenye ushindani,” amesema Gamondi.
Kauli hiyo imeongeza matumaini kwa mashabiki wa soka nchini, huku Taifa Stars ikiendelea na maandalizi ya mwisho kuelekea mashindano makubwa ya bara la Afrika.