INAELEZWA kuwa kiungo mshambuliaji wa Simba SC yupo kwenye hesabu za mabosi wa Mbeya City ambao wanahitaji huduma yake.
Awesu kwa msimu wa 2025/26 hajawa na nafasi kikosi cha kwanza kwenye mechi za ushindani jambo linalofanya kiwango chake kutokuwa imara.
Ikumbukwe kwamba aliibuka ndani ya Simba SC akitokea Klabu ya KMC huko alikuwa ni chaguo la kwanza na alikuwa na uhakika wa namba.
Tetesi zinaeleza kuwa Mbeya City wametuma ofa kwa Simba SC wakihitaji huduma ya mchezaji huyo kwa mkopo hivyo makubaliano yakienda vizuri atakuwa kwenye changamoto mpya.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.