Bayern Munich imeonyesha ubabe katika dimba la Allianz Arena baada ya kutoka nyuma 1-0 na kuibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Sporting Lisbon kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kichekesho kilitokea dakika ya 54 baada ya Joshua Kimmich kujifunga na kuwapa Sporting uongozi, lakini Bayern ikarejea mchezoni kwa nguvu na kufunga mabao matatu ndani ya dakika 12.
FT: Bayern Munich π©πͺ 3-1 π΅πΉ Sporting Lisbon
β½ 65β Gnabry
β½ 69β Karl
β½ 77β Tah
β½ 54β Kimmich (og)
Ushindi huo unaendeleza rekodi nzuri ya Bayern ya kuwa wagumu kupinduliwa nyumbani katika michezo ya Ulaya.