Mnyama apoteza mbele ya Azam FC kwa kupigwa 2-0

Simba SC 0-2 Azam FC ubao umesoma hivyo Uwanja wa Mkapa mara baada ya dakika 90 kwenye msako wa pointi tatu muhimu.

Wababe hawa wawili kwenye Mzizima Dabi kila mmoja alikuwa kwenye hesabu za kusaka ushindi na mwisho matajiri wa Dar, Azam FC wamewatuliza wenyeji wao.

Mabao mawili yote yamefungwa kipindi cha pili ikiwa ni dakika 5 zimesalia mpira kugota mwisho kwa timu hizo mbili kupambania ushindi.

Jephte Kitambala alifungua ukurasa wa mabao dakika ya 81 kipindi cha pili na kamba ya pili ilifungwa na Idd Nado dakika ya 89 ya mchezo.

Huu ni mchezo wa kwanza kwa Simba SC kupoteza ndani ya uwanja katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/26.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.