Stade Malien vs Simba SC ni leo CAF Champions League

Stade Malien vs Simba SC ni leo CAF Champions League ikiwa ni mchezo wa hatua ya makundi kwa wababe hawa kuwa uwanjani.

Simba SC imetoka kupoteza mchezo wake wa kwanza ikiwa nyumbani ambapo ilifungwa bao 1-0 dhidi ya Petro de Luanda ikiwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa leo unakuwa wa pili kwa timu hizi mbili kusaka pointi tatu ndani ya uwanja msimu wa 2025/26 ikiwa ni katika kutafuta tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC mara baada ya kumaliza mkutano mkuu wa mwaka 2025 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee amewaomba mashabiki kuiombea dua timu hiyo ipate matokeo mazuri.

“Baada ya kumaliza mkutano mkuu kwa sasa ni muda wa kila shabii kuiombea dua njema timu yetu ipate matokeo mazuri kwenye mchezo wetu wa kimataifa,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.