MARA baada ya mwisho wa reli Kigoma Novemba 28 kutopatikana mbabe ndani ya dakika 90 kazi inatarajiwa kuendelea leo kwa wababe wengine uwanjani.
Kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma ubao ulisoma Mashujaa FC 0-0 Dodoma Jiji wababe hawa wakigawana pointi mojamoja.
Pamba Jiji leo Novemba 29,2025 watashuka Uwanja wa Kirumba kusaka pointi tatu muhimu ndani ya uwanja katika mchezo wa NBC Premier League.
Ikiwa nafasi ya pili na pointi 12 Pamba Jiji FC itamenyana na KMC ambao hawa wanaburuza msimamo wakiwa na pointi4 baada ya mechi 4 msimu wa 2025/26.
Mbali na mchezo huo, Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya 12 vs TRA United nafasi ya 11 unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar.