Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuahirisha hafla ya utoaji wa Tuzo za Msimu wa 2024/2025 ambayo ilipangwa kufanyika tarehe 5 Desemba 2025.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, uamuzi huo umetokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao kwa sasa, hivyo kuwalazimu kusogeza mbele tukio hilo muhimu la kimichezo.
“Mara tarehe mpya itakapopangwa mtafahamishwa mara moja,” taarifa hiyo imeeleza.
