Ratiba ya NBC Premier League Novemba 26,2025

NBC Premier League 2025/26 bado moto unaendelea ikiwa ni raundi ya 8 kwa timu kushuka uwanjani kusaka pointi tatu muhimu.

Mechi kali tatu zinatarajiwa kuchezwa leo ya kwanza itakuwa Coastal Union vs Mbeya City saa 8:00 mchana, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Fountan Gate vs Tanzania Prisons saa 10:15 jioni, Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara.

Funga kazi ni JKT Tanzania vs TRA United saa 12:30 jioni Uwanja wa Mej.. Jen Isamuhyo.

Vinara wa ligi kwa sasa ni Pamba Jiji FC wakiwa na pointi 12 baada ya mechi 7 ndani ya ligi. Nafasi ya mwisho ni KMC FC ambayo imekusanya pointi 4 baada ya mechi 8.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.