Pedro awapa tano wachezaji Yanga SC, kazi inaendelea CAF Champions League

Pedro Goncalves, Kocha Mkuu wa Yanga SC ameweka wazi kuwa wachezaji walijituma kwenye mchezo wa kwanza anaamini watapambana katika mchezo ujao.

Ikiwa nyumbani kwenye mchezo wa ufunguzi, Yanga SC ilipata ushindi wa bao 1-0 AS Far Rabat mchezo wa makundi na kukomba pointi tatu mazima.

Kituo kinachofuata CAF Champions League itakuwa ugenini dhidi ya JS Kabylie ya Algeria. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku Novemba 28,2025. Utakuwa ni mchezo wa kwanza hatua ya makundi ugenini ikiwa ni raundi ya pili, Uwanja wa Hocine Ait Ahmed.

Rekodi zinaonyesha kuwa kati ya mechi 8 ambazo JS Kabylie alicheza akiwa nyumbani alipata ushindi katika mechi 7

Yanga SC katika mechi 4 zilizopita ushindi ilikuwa ni asilimia 100.

Msimamo wa kundi B

1. Al Ahly mechi 1 pointi 3
2.Yanga SC mechi 1 pointi 3
3. AS Far Rabat mechi 1 pointi 0
4. JS Kabylie mechi 1 pointi 0

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.