Simba SC wakali wa Backpass CAF Champions League nyumbani

Simba SC katika mchezo wa CAF Champions League dhidi ya Petro de Luanda waliongoza rekodi ya kupiga pasi nyingi kwenye lango lao ndani ya dakika 90 wakiwa nyumbani, Uwanja wa Mkapa.

Rekodi zinaonyesha kuwa Simba SC ilipiga jumla ya back pass 66 huku wageni Petro de Luanda wakipiga jumla ya back pass 56.

Katika mchezo huo Novemba 23,2025 hakuna timu iliyopata pigo la kona ndani ya dakika 90 hivyo hakukuwa na mashambulizi ya nguvu kila timu ilikuwa inategea.

Ni pasi 324 Simba SC ilipiga huku wapinzani wao Petro de Luanda wakipiga pasi 241.

Simba SC wakiwa ndani ya box walipiga mashuti 6 na Petro de Luanda shuti moja ambalo lilikuwa goli.

Mchezaji wa kwanza kugusa mpira dakika ya kwanza ya mchezo alikuwa ni Joshua Mutale wa Simba SC.

Nafasi kubwa za wazi ambazo Simba SC ilipata na kukosa ni tatu wapinzani Petro de Luanda hawakupata Big Chance…

FT: Simba SC 0-1 Petro de Luanda.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.