Simba Kuondoka Alfajiri Novemba 27 Kwenda Mali kwa Mchezo wa Ligi ya Mabingwa

Klabu ya Simba inatarajiwa kuanza safari yake alfajiri ya Alhamisi, Novemba 27, kuelekea nchini Mali kwa ajili ya mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Stade Malien.

Wekundu wa Msimbazi watamenyana na wenyeji Stade Malien mnamo Novemba 30, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, mchezo ambao utapigwa majira ya saa 1 usiku.