CAF Cofederation Cup ratiba ipo namna hii

CAF Cofederation Cup ratiba bado inaendelea kupasua anga ambapo wawakilishi wa Tanzania kwenye hatua za makundi watakuwa nyumbani katika mechi za raundi ya pili.

Singida Black Stars na Azam FC hizi zitakuwa nyumbani kusaka pointi tatu muhimu baada ya mechi zilizopita za ufunguzi kupoteza ugenini.

Ijumaa Novemba 28, Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Florent Ibenge watakuwa Uwanja wa New Amaan Complex vs Wydad Casablanca.

Mechi hii itachezwa kuanzia saa 1:00 usiku na kuruka mbashara kupitia AzamSports2HD.

Jumapili Novemba 30, Singida Black Stars chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi watakuwa Uwanja wa New Amaan Complex vs StellenBosch ya Afrika Kusini.

Mechi itachezwa kuanzia saa 1:00 usiku na kuruka mbashara kupitia AzamSports3HD.