Simba SC kwenye mtihani mwingine CAF Champions League

Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza hatua ya makundi dhidi ya Petro de Luanda wakiwa Uwanja wa Mkapa mtihani mwingine unafuata kwa mnyama ugenini.

Kwa sasa kituo kiachofuata ni Novemba 28,2025 ambapo watakuwa ugenini mchezo wa pili hatua ya makundi.

Itakuwa ni Stade Malien vs Simba SC, kwenye msako wa pointi tatu muhimu saa 1:00 usiku kwa wababe hawa wawili ambao mechi zao zilizopita wote hawakupata pointi tatu muhimu uwanjani.

Simba SC inaburuza kundi D ikiwa haijakusanya pointi kwa kuwa mchezo wa ufunguzi ilifungwa bao 1-0.

Stade Maline ililazimisha sare ya bila kufungana na wapinzani wao Esperence ST ikiwa ugenini hivyo ilivuna pointi moja.

Wapinzani wa Simba SC wamekuwa wakitumia mara nyingi kipindi cha kwanza kumaliza mchezo ambapo kwenye mechi kati ya 7 ambazo walicheza rekodi zinaonyesha kwamba 6 walipata ushindi kipindi cha kwanza.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.