Farhan Kihamu Awasha Moto: ‘Negative Yangu Kwa Yanga Ni Facts – Video

Mwanahabari na mchambuzi wa soka nchini, Farhan Kihamu (@jr_farhanjr), ameibua mjadala mpya mitandaoni baada ya kueleza kuwa kila anapoandika jambo la upande hasi (negative) kuhusu klabu ya Yanga, basi taarifa hiyo huwa ni ya kweli na imefanyiwa uhakiki wa kina.

Kihamu ametoa kauli hiyo kupitia mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye YouTube ya Global TV, akisema uandishi wake hauongozwi na ushabiki bali ukweli, weledi na majukumu yake kama mwandishi wa habari.

“Mimi siandika tu kwa hisia. Nikisema jambo kuhusu Yanga—hata kama ni negative—basi nimehakiki. Ni kweli tupu,” alisema Kihamu.

Kauli hiyo imepokelewa kwa mitazamo mseto kutoka kwa mashabiki wa soka, hasa kutokana na ukweli kwamba Yanga ni moja ya klabu zenye mashabiki wengi na wenye ushawishi mkubwa nchini.

Katika mahojiano hayo, yaliyosimamiwa na mtangazaji Mohamed Hussein (@mohusein_15), Kihamu alisisitiza kuwa jukumu la mwanahabari ni kuweka wazi ukweli na si kupendelea upande wowote, akibainisha kuwa hata taarifa zenye utata lazima ziwekwe hadharani ikiwa zina maslahi kwa umma.

Wapenzi wa soka na wadau wengine wametakiwa kufuatilia mahojiano hayo kamili kupitia YouTube ya Global TV, wakihimizwa ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili kuendelea kupata habari za uhakika kila siku.