Wanaowania Tuzo za TFF 2024/25 Wapo Hapa… Tuzo Kutolewa Desemba 5, 2025, The Super Dome, Dar

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefahamisha wanaowania Tuzo za Msimu wa Ligi Kuu 2024/2025, huku tukitarajia watakaoibuka washindi rasmi Desemba 5, 2025 katika ukumbi wa The Super Dome, Dar es Salaam.

Wanaowania Wakuu wa Tuzo za Ligi Kuu NBC:

Mchezaji Bora: Dickson Job (Yanga), Pacome Zouzoua (Yanga), Maxi Nzengeli (Yanga), Jean Ahoua (Simba), Feisal Salum (Azam)

Kipa Bora: Djigui Diarra (Yanga), Moussa Camara (Simba), Patrick Munthali (Mashujaa FC)

Kiungo Bora: Feisal Salum (Azam), Jean Ahoua (Simba), Pacome Zouzoua (Yanga)

Beki Bora: Antony Urbain Tra Bi (Singida Black Stars)

Waamuzi Bora: Ahmed Arajiga, Saad Mrope na Abdallah Mwinyimkuu

Tuzo za Ligi ya Wanawake: Donisia Minja (JKT Queens), Esther Maseke (Bunda Queens), Jeannine Mukandayisenge (Yanga Princess), Jentrix Shikangwa (Simba Queens), Stumai Abdallah (JKT Queens)

Tuzo hizi ni sehemu ya jitihada za TFF kuwatambua wachezaji, makocha na waamuzi waliotoa mchango mkubwa msimu huu. Mashabiki wanatarajiwa kufuatilia tukio la Desemba 5 kwa hafla ya kipekee itakayowakutanisha wadau wa mpira wa miguu wa Tanzania.