Simba SC yapiga hesabu kumalizana na Petro de Luanda

Simba SC vs Petro de Luanda Novemba 23,2025 Uwanja wa Mkapa ikiwa ni mchezo wa kwanza hatua ya makundi, uongozi wa wenyeji umepiga hesabu kuvuna pointi tatu.

Kutoka kundi D mchezo wa kwanza Simba SC itakuwa nyumbani na tayari Novemba 20,2025 walizindua jezi mpya ambazo zitatumika kwenye mashindano hayo zikiwa na nembo ya CAF.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa mashabiki ni muhimu kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo ili kuwaongezea nguvu wachezaji wakiwa uwanjani.

“Ni mchezo mgumu hasa kulingana na hatua ambayo tupo kwa sasa kila timu inatafuta pointi tatu. Tupo nyumbani kikubwa ambacho tunahitaji ni kuona tunapata matokeo mazuri.

“Mashabiki wanatupa nguvu yakubaki hapa na tutakuwa Uwanja wa Mkapa, mchezo wetu wenyewe na mashabiki wanajua furaha ipo kwenye ushindi hilo ni jukumu la wachezaji kutupambania mpaka mwisho,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.