Yanga SC kuzindua uzi mpya leo Novemba 19,2025

RASMI uongozi wa Yanga SC umetangaza kuwa utazindua uzi mpya maalumu kwa ajili ya mechi za CAF Champions League leo Novemba 19,2025.

Yanga SC inapeperusha bendera ya Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika ipo hatua ya makundi na mchezo wa kwanza unatarajiwa kuchezwa Novemba 22, 2025 Uwanja wa New Amaan Complex dhidi ya FAR Rabat ya Morocco.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amesema kuwa wameamua kufanya hivyo kutokana na maombi kutoka kwa mashabiki kuhitaji kuona wanapata muda wakutosha kununua jezi kabla ya mchezo wa kwanza.

“Awali tulitangaza kuwa uzinduzi itakuwa ni Novemba 20,2025 siku ya Alhamisi lakini kutokana na maombi kutoka kwa mashabiki kuona wanapata muda kununua jezi basi tumeamua kuzindua mapema.

“Novemba 19,2025 tutafanya uzinduzi maalumu wa jezi yetu mpya kwa mashindano ya kimataifa hivyo kila shabiki awe tayari na nashauri mzigo uchukuliwe mapema zitakapozinduliwa,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.