Kuwaona Yanga SC vs FAR Rabat CAF Champions League ni buku tano tu

Yanga SC va FAR Rabat ya Morocco CAF Champions League mchezo unatarajiwa kuchezwa Novemba 22,2025 Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Tayari Yanga SC ambao ni wawakilishi wa Tanzania kwenye anga la kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika wapo visiwani Zanzibar kwa maandalizi ya mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni.

Kwa 5,000 yaani buku tano unapata fursa ya kuwaona wababe hawa wawili katika msako wa pointi tatu kwenye mchezo wa makundi.

Maeneo na bei zake zipo namna hii

Saa ni 5,000

Orbit-5,000

Urusi-10,000

Wings-20,000

VIP-30,000

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo kushuhudia burudani na kuwapa kazi wachezaji kutafuta ushindi.

“Mashabiki ni kazi yetu kwenye mchezo huu kujitokeza kwa wingi na kushangilia bila kuchoka ili kuona wachezaji wanapata kazi zaidi kutafuta matokeo uwanjani,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.