AS Maniema vs Azam FC Novemba 23,2025 Kombe la Shirikisho Afrika

AS Maniema vs Azam FC Novemba 23,2025 Kombe la Shirikisho Afrika ni mchezo wa kwanza katika hatua ya makundi kwa wawakilishi wa Tanzania katika anga la kimataifa.

Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Flolent Ibenge Novemba 19,2025 msafara unatarajia kukwea pipa kueleka DR Congo kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.

Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema kuwa wanatambua wapo katika kundi gumu hivyo maandalizi ambayo yanafanyika ni maalumu kwa ajili kueleta ushindani.

“Tupo kwenye kundi gumu hili niliweka wazi tangu awali hivyo hakuna timu ambayo tunaichukulia kwa wepesi kikubwa ni kuona kwamba tupo tayari.

“Mchezo wetu ugenini utakuwa ni wa ufunguzi tunaamini kwamba tutafanya vizuri na msafara unatarajiwa kuondoka Tanzania Novemba 19,2025 asubuhi,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.