Saudi Arabia Yajenga Uwanja Wa Mpira Angani – Una Vituo Vya Burudani Na Mazoezi…

Katika siku za hivi karibuni, Saudi Arabia imekuwa ikifanya juhudi kubwa kujiweka kwenye ramani ya dunia kama kiongozi katika maendeleo ya michezo, na mojawapo ya miradi mikubwa zaidi ni ujenzi wa uwanja wa mpira wa mawinguni, ambao unalenga kuwa kivutio cha kipekee katika sekta ya michezo duniani.

Uwanja huu, unaojulikana kama Neom Sky Stadium au The Cloud Stadium, siyo tu kwamba ni hatua muhimu katika mpango wa Saudi Arabia wa ‘Vision 2030,’ lakini pia ni mfano wa ubunifu na teknolojia katika ujenzi wa viwanja vya michezo.

Global TV imekuandalia makala ya jinsi ujenzi wa uwanja huu ulivyoanza, eneo lake, ukubwa na uwezo wa kubeba watu, na namna ambavyo Saudi Arabia wameweza kutimiza ndoto hii ya kipekee.