Taifa Stars Yapoteza 4-3 Dhidi Ya Kuwait, M’mombwa Awaka Mara Mbili
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imepoteza mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa kalenda ya FIFA kwa mabao 4-3 dhidi ya Kuwait, katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Al Salaam, Cairo – Misri. Tanzania ilianza vizuri mchezo huo na kupata bao la mapema dakika ya 7 kupitia Charles M’mombwa, kabla ya Allarakhia kuongeza la pili…