TIMU ya Taifa ya Tanzania inayofundishwa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi Novemba 15,2025 itakuwa kazini kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Kuwait.
Tayari kikosi cha Tanzania kipo nchini Misri kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo huo miongoni mwa hao ni Mohamed Hussen Zimbwe Jr, Kelvin John, Shomari Kapombe, Bakari Nondo.
Kelvin John amesema: “Tutatumia mchezo huu kuwa ni kipimo kwa mechi zijazo za AFCON kwa kuwa siku sio nyingi tutaanza. Makosa yetu na pale ambapo tutafanya vizuri tutaangalia kupitia mchezo huu ambao tunaamini utakuwa ni mgumu,”.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Al Salam, jijini Cairo ukiwa ni mchezo maalumu ambao upo kwenye kalenda ya FIFA.
Gamondi amesema anaamini vijana watafanya kazi kubwa kwenye mchezo huo muhimu kupata matokeo mazuri uwanjani.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.
Soccer Football - LaLiga - Atletico Madrid v Espanyol - Metropolitano, Madrid, Spain - November 6, 2022 Atletico Madrid's Joao Felix scores their first goal REUTERS/Juan Medina