Simba SC Yapangwa Kundi D na Miamba ya Tunisia, Angola na Mali Ligi ya Mabingwa Afrika

Wekundu wa Msimbazi Simba wamepangwa Kundi D la Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya Makundi ikiwa na miamba ya Tunisia Espérance Sportive de Tunis, Atlético Petróleos de Luanda ya Angola na Stade Malien ya Mali.

Droo ya Michuano hiyo imepangwa leo mchana Mjini Cairo, Misri.