KUELEKEA kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Yanga SC vs Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex, benchi la ufundi la Wananchi limebainisha ugumu ulipo.
Timu hizo mbili zinatarajiwa kukutana saa 10:00 jioni kwenye msako wa pointi tatu muhimu ikiwa ni mchezo wa ligi msimu wa 2025/26.
Patrick Mabedi, kocha msaidizi wa Yanga SC amebainisha kuwa mchezo huo hautakuwa mwepesi kwa kuwa kila timu inahitaji matokeo mazuri.
Mabedi amesema wataingia uwanjani kwa tahadhari kwa ajili ya mchezo huo muhimu na lengo ni kutafuta matokeo mazuri uwanjani.
“Kila mchezo una ugumu wake, kwenye ligi lazima ushindani uwepo na tunaheshimu kila mpinzani. Tunahitaji kuwa makini sana kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar. Tunachokifanyia kazi mazoezini kwa sasa ni kuhakikisha wachezaji wanatumia vyema kila nafasi wanayoipata,”.
Kwenye msimamo Yanga SC imecheza mechi 2 ipo nafasi ya 13 na pointi 4 inakutana na Mtibwa Sugar ambayo imecheza mechi 4 ikiwa na pointi 5 nafasi ya 8.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.