Historia! Tanzania Yaweka Rekodi CAF – Timu Nne Zatinga Makundi

Kwa mara ya kwanza katika historia, Tanzania imefanikiwa kupeleka timu nne kwenye hatua ya makundi ya michuano inayoendeshwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Baada ya Simba SC kupata ushindi wa jumla wa 3-0 dhidi ya Nsingizini Hotspurs FC ya Eswatini, Wekundu wa Msimbazi wamejiunga rasmi na Yanga SC katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).

Hii inamaanisha Tanzania sasa inawakilishwa na timu mbili kwenye CAF Champions League (Simba SC na Yanga SC), na timu mbili nyingine — Singida Black Stars na Azam FC — kwenye Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup).