Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL)inaendelea tena leo Oktoba 25, 2025 kwa mechi saba kwenye viwanja mbalimbali huku wawakilishi wa Tanzania, Young Africans Sc wakitupa karata yao ya pili kwenye hatua ya pili dhidi ya vigogo wa Malawi, Silver Strikers Fc katika dimba la Benjamin Mkapa saa 11:00 jioni.
Wananchi wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa nyuma baada ya kipigo cha 1-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza ambapo kiungo wa Silver Strikers, Uchizi Vunga alifanya ‘mabalaa’ kwenye mchezo huo akihusima kwenye shambulizi lililozaa bao hilo pekee.
Yanga Sc wanahitaji walau ushindi wa 2-0 au ushindi wowote wa tofauti ya magoli mawili au zaidi ili kutinga hatua ya makundi ya CAFCL msimu wa 2025/26. Ushindi wa 1-0 utapelekea mchezo kuamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.
17:00 Young Africans 🇹🇿 vs 🇲🇼 Silver Strikers (Agg. 0-1)
🏟️ Benjamin Mkapa
MECHI ZINGINE: #CAFCL
16:00 Orlando Pirates 🇿🇦 vs 🇨🇩 St Eloi Lupopo (Agg. 0-3)
18:00 Rivers United 🇳🇬 vs 🇲🇿 Black Bulls (Agg. 0-1)
19:00 Petro Atletico 🇦🇴 vs 🇨🇮 Stade d’Abidjan (Agg. 2-0)
20:00 Al Ahly 🇪🇬 vs 🇧🇮 Aigle Noir (Agg. 1-0)
21:00 JS Kabylie 🇩🇿 vs 🇹🇳 US Monastir (Agg. 3-0)
22:00 FAR Rabat 🇲🇦 vs 🇬🇳 Horoya (Agg. 1-1)