Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Hakim Ziyech, amefikia makubaliano ya kujiunga na klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Kwa mujibu wa mwandishi maarufu wa masuala ya usajili, Fabrizio Romano, Ziyech amesaini kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Al-Duhail ya Qatar mwishoni mwa msimu uliopita.
Ndani ya kikosi cha Wydad, Ziyech ataungana na kiungo wa zamani wa Yanga SC, Stephane Aziz Ki, ambaye pia amejiunga na klabu hiyo hivi karibuni.