Silver Strikers FC vs Yanga SC CAF Champions League unatarajiwa kuchezwa leo Oktoba 18, 2025 Uwanja wa Bingu- Malawi kwa wababe wawili kusaka ushindi uwanjani.
Baada ya kete ya leo kituo kinachofuata itakuwa ni Yanga SC vs Silver Strikers FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 25, 2025 huu ni mchezo ambao utaamua mshindi atakeyetinga hatua ya makundi.
Aziz Andambwile kiungo wa Yanga SC amesema wapo vizuri kuwakabili Silver Strikers ya Malawi kwenye mchezo wa ugenini na benchi la ufundi limewapa maelekezo yakufanyia kazi.
Ikumbukwe kwamba kwenye mechi za awali Andambwile alifunga magoli mawili alianza ugenine na moja alifunga Uwanja wa Mkapa walipotinga hatua inayofuata kwa jumla ya magoli 5-0 Wiliete vijana wa Angola.
Andambwile amesema: “Tunaamini mchezo utakuwa mgumu, wachezaji tumejiaanda vizuri kwa asilimia 90 tupo tayari ili kupata matokeo mazuri katika mchezo wetu.
“Kuna namna ambavyo tumepewa maelekezo kwa ajili ya mchezo wetu. Timu ambayo tunacheza nayo ni nzuri na tunaamini mchezo utakuwa mzuri nasi wachezaji tupo tayari,” amesema Andambwile.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.