Nsingizini Hotspurs vs Simba SC, Maema, De Reuck wapewa angalizo

Nsingizini Hotspurs vs Simba SC, mchezo unaofuata kwa Simba SC katika anga la kimataifa ikiwa ni CAF Champions League unatarajiwa kuchezwa ugenini.

Hii ni kete ya kwanza kimataifa kwa Meneja Mkuu wa Simba SC, Dimitar Pantev huku wachezaji wapya wa timu hiyo ikiwa ni Neo Maema, De Reuck wakipewa angalizo kuhakikisha kwamba wanapambana kupata matokeo mazuri.

Ikumbukwe kwamba mshindi wa jumla katika mchezo huu atakwenda hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amebainisha kuwa wachezaji wote wana kazi kuelekea mchezo ujao kimataifa kuhakikisha wanaendeleza utamaduni wa timu hiyo kupata matokeo mazuri.

“Wachezaji wapya baadhi De Reuck na Maema wanaifahamu historia waliyoikuta Simba ya ushiriki wetu wa kimataifa na siyo hao pekee pia wachezaji wengine kama yupo hafahamu umuhimu wa kufuzu makundi lazima atambue na kuendeleza ile historia,”

Mchezo wa Nsingizini Hotspurs vs Simba SC ni Oktoba 19 2025 na ule wa marudiano ni Simba SC vs Nsingizini Hotspurs, Oktoba 24,2025, kwenye  CAF Champions League.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.