Romain Folz aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga SC kwenye mechi saba rasmi amefukuzwa Oktoba 18,2025 kwenye nafasi hiyo.
Mara baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Silver Strikers, Yanga SC wametoa taarifa kuhusu kuvunja mkataba na Folz.
Mchezo wa leo akiwa benchi baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Bingu-Malawi umesoma Silver Strikers 1-0 Yanga SC ikiwa ni Ligi ya Mabingwa Afrika mchezo wa kusaka hatua ya kutinga hatua ya makundi.
Taarifa kutoka Yanga SC hii hapa
“Uongozi wa Young African Sports Club unapenda kuutarifu Umma kuwa, umevunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza, Romain Folz.
“Uongozi wa Young African Sports Club unamshukuru kocha Romain Folz kwa mchango wake ndani ya klabu yetu na unamtakia kila la kheri katika majukumu yake yanayofata.
“Katika kipindi hiki kikosi chetu kitakuwa chini ya kocha msaidizi Patrick Mabedi huku mchakato wa kutafuta kocha mkuu ukiendelea,” ilieleza taarifa hiyo.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.