Msafara wa Simba SC ndani ya Afrika Kusini

WAWAKILISHI wa Tanzania, Simba SC chini ya Meneja Mkuu Dimitar Pantev wanakibarua kuelekea mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika na mapema Oktoba 16 2025 walianza safari kuelekea Eswatini.

Tayari Msafara wa kikosi cha Simba SC wenye wachezaji 22 umewasili salama Afrika Kusini ikiwa ni njia kwa ajili ya kuelekea Eswatini.

Safari ya Simba SC kuelekea Eswatini itaendelea jioni ya leo kwa ajili ya kufika mahali ambapo mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwa wababe hao kusaka ushindi.

Haya ni maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa Jumapili, Oktoba 19 dhidi ya Nsingizini Hotspurs ya Eswatini.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.