MABINGWA wa Ligi Kuu ya Eswatini 2024/25 Nsingizini Hotspurs chini ya Kocha Mkuu, Mandla Qhogi wanatarajiwa kukutana na Simba SC, Oktoba 19 2025. Huu utakuwa mchezo wa raundi ya pili unatarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa taifa wa Somhlolo.
Timu hiyo ilipenya hatua hiyo kwa kuwafungashia virago Simba Bhora katika hatua ya awali. Ni kwa jumla ya penalti 4-2 baada ya wote kufungana bao 1-1 katika kila mchezo. Kila timu ilipata ushindo nyumbani.
Katika mchezo wa kwanza Septemba 21 2025 ilikuwa Simba Bhora 1-0 Nsingizini Hotspurs. Mchezo wa pili Septemba 28 2025 ilikuwa Nsingizini Hotspurs 1-0 Simba Bhora.
Katika mchezo ulioamua mshindi atakayetinga hatua ya pili, Nsingizini Hotspurs walipata goli dakika za jioni. Zikiwa zimesalia dakika tatu mpira kukamilika katika muda wa nyongeza. Ilikuwa dakika ya 90+1 Nkosingiphile Shongwe alipachika goli ambalo likapelekea mshindi atafutwe kwa penalti.
Kwenye mapigo ya penalti ilikuwa Nsingizini Hotspurs 4-2 Simba Bhora hivyo wakafungashiwa virago jumlajumla mabingwa wa Zimbabwe. Simba Bhora wao jukumu lao ilikuwa ni kulinda ushindi waliopata nyumbani wakakwama.
Kocha Mkuu wa Simba Bhora aliliona mapema ambapo Luphahla alisema kuwa licha ya kupata ushindi watakutana na ugumu wakiwa ugenini.
Kocha Qhogi aliweka wazi kuwa wataweka ugumu wakiwa nyumbani kwa kuwa wanatambua ubora wa wapinzani wao.
Kuelekea mchezo wao dhidi ya Simba SC tayari maandalizi yanaendelea kwa wababe hawa katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.