Rais wa Klabu ya Yanga SC ambaye ni Mwenyekiti wa Vilabu barani Afrika(ACA), Eng. Hersi Said ameteuliwa na Shirikisho la Soka Duniani, (FIFA) kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano yote ya vilabu ya Wanaume Duniani.
Nafasi hiyo atadumu nayo kwa muda wa miaka minne kuanzia 2025-2029. Oktoba 2 maamuzi yalichukuliwa na FIFA na taarifa ilitumwa Oktoba 7.
Injinia kwa sasa anasubiri taarifa nyingine ambayo atatumiwa kwa njia ya email ili ajaze CV yake tayari kwa kuanza majukumu mapya kwenye ulimwengu wa mpira.
Kutokana na majukumu hayo mapya ambayo ni makubwa anakuwa ni mtu wa kwanza kutoka Afrika mashariki na kati kuingia kwenye kamati kubwa ya mpira Ulimwenguni.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.