MENEJA Mkuu wa Simba SC, Dimitar Pantev ameanza kazi kwa ajili ya kuwapa mbinu wachezaji wa timu hiyo kuelekea kwenye mechi za ushindani msimu wa 2025/26.
Mchezo wake wa kwanza mbinu zake zinatarajiwa kutumika kimataifa katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika mrithi wa mikoba ya Fadlu Davids ambaye alitua Bongo Oktoba 4 2025.
Mchezo wake wa kwanza unatarajiwa kuwa Oktoba 17 ambapo Simba SC itakuwa ugenini kusaka ushindi dhidi ya Nsingizini Hotspurs ya Eswatini wakiwa ugenini.
Oktoba 24-25 Simba SC vs Nsingizini huu unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ambapo mshindi wa jumla atatinga hatua ya makundi.
Novemba 2 2025, Simba SC vs Azam FC, Uwanja wa Mkapa utakuwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara ya NBC ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa Pantev.
Kariakoo Dabi itakuwa ni funga mwaka ndani ya 2025 kwa Simba SC. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Desemba 13 2025, Yanga SC vs Simba SC, Uwanja wa Mkapa.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.