
TFF Yamsimamisha Mchezaji wa Yanga Princess Kupisha Uchunguzi wa Jinsia
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesimamisha kwa muda mchezaji wa klabu ya Yanga Queens, Princess Jeanine Mukandiyisenga, raia wa Rwanda, kupisha uchunguzi wa kina kuhusu jinsia yake. Hatua hii imekuja baada ya sintofahamu kuibuka mitandaoni na katika baadhi ya duru za michezo, ambapo mashabiki na wadau wameanza kuhoji hali halisi ya jinsia ya mchezaji huyo,…