UNAZIKUMBUKA zile kazi ambazo zilikuwa zinapigwa kila kona kutoka kwa kijana Samir wa Kinyulinyuli? Hapa tunazungumzia muziki ule wa Bongo Fleva?
Mbali na Kinyulinyuli ambayo ilibamba na bado inaishi kwenye maskio ya wapenda muziki aliachia Darling ambayo nayo ni kali sasa habari ikifukie kwa sasa kijana hutamskia kwenye utunzi wa aina hiyo kwa kuwa ameamua kuimba Muziki wa Injili.
Samir amesema kuwa amemua kufanya hivyo kwa kuwa ni wakati sahihi wa kuimba nyimbo za kumtukuza na kutangaza sifa za Mungu.
“Kuna kazi mpya ambazo zinakuja ambazo ni za Gospel tu ninakaribia kutoa EP yangu ya nyimbo hizo kwa. Kwa hiyo wale mashabiki waliokuwa wakifuatilia kazi zangu kwa sasa wategemee kunisikia kwenye mziki wa injili.
“Nimeona huu ni wakati sahihi mimi kuimba nyimbo za kumtukuza na kumsifu Mungu na kutangaza sifa zake na kuwafanya watu wasikate tamaa mpaka kufikia kujiua, wajue Mungu ndio suluhisho la kila tatizo la mwanadamu.
“Hivyo basi wamkimbilie Mungu kwenye kila aina ya mapito yao na wamuabudu Mungu maana lengo la Mungu kutuumba ili tumuabudu yeye,”.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.