Baada ya Kicheko sasa ni Popote kutoka wa SYC

BAADA ya uzinduzi wa Albamu ya Kicheko kutoka kwa Sinza Youth Choir, (SYC)  kutoka KKKT-DMP  Usharika wa Sinza, sasa ni uzinduzi wa wimbo mpya unaoitwa Popote.

Hii ni kazi nyingine ambayo malengo makubwa ni kuitangaza injili mjini na vijijini kwa njia ya uimbaji ikiwa ni mwendelezo wa kazi nyingine mpya kutoka SYC.

Septemba ilikuwa ni njema kwa kila mmoja na Mungu ni mwema jina la Popote litawafakia wengi hivyo unaombwa kuwa tayari kuusikiliza na kuupokea wimbo wa Popote.

Wimbo huu mpya ni utunzi wa Mwalimu Baraka hakika utakuwa ni baraka kwako pia na jirani bila kusahau yule ambaye utamwambia ausikilize akiwa popote ulimwenguni.

Ni Oktoba 3 2025 kazi hii mpya inatarajiwa kuwa tayari kwa utambulisho wake ambapo kila kitu kuhusu utayarishaji wa wimbo mpya upo vizuri ni suala la muda tu kutambulishwa.

Ikumbukwe kwamba Albamu ya Kicheko kwa sasa inapatikana kwenye mitandao ya kijamii ikiwa ni YouTube, AudioMac ilitambulishwa rasmi Desemba 3 2023 bado inaendelea kufanya kazi katika kutoa injili mjini na vijijini.

Bado Albamu ya Kicheko ipo kwa ajili yako na ukihitaji unakaribishwa KKKT Sinza Kumekucha kwa ajili ya kupata baraka hizi za Mungu wa mbinguni, hakika utabarikiwa na usipange kukosa kazi mpya ya Popote, Oktoba 3 2025.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.