Mshambuliaji wa zamani wa Young Africans SC, Fiston Kalala Mayele, ameendelea kuonyesha makali yake barani Afrika na duniani baada ya kufunga mabao matatu (hat-trick) yaliyoipeleka Pyramids FC ya Misri hatua inayofuata ya michuano ya Kombe la Mabara la FIFA.
Pyramids FC imeiondoa Al Ahli Saudi ya Saudi Arabia kwa jumla ya mabao 3β1, licha ya wapinzani wao kuwa na wachezaji nyota kama Riyad Mahrez (winga wa zamani wa Manchester City), Franck Kessie (kiungo wa zamani wa Barcelona), na Ivan Toney (mshambuliaji wa zamani wa Brentford), ambaye alifunga bao pekee la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati dakika ya 45.
Mayele alifunga bao la kwanza dakika ya 21, kabla ya kuongeza mawili ya kuvutia dakika ya 71 na 75, na kupelekea Pyramids kuandika historia katika michuano hiyo mikubwa ya FIFA.
Kwa ushindi huo, Pyramids FC sasa itamenyana na mabingwa wa Amerika Kaskazini/Kusini, ambapo mshindi wa mchezo huo atakutana na mabingwa wa Ufaransa, Paris Saint-Germain (PSG), katika fainali.
Mbali na michuano ya Kombe la Mabara, Pyramids FC pia inakabiliwa na jukumu jingine wiki ijayo, itakaposafiri nchini Rwanda kuvaana na APR FC katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Matokeo ya Mwisho (FT):
Al Ahli Saudi πΈπ¦ 1β3 πͺπ¬ Pyramids
β½ 21β Mayele
β½ 45β Toney (pen.)
β½ 71β Mayele
β½ 75β Mayele