Bingwa wa Dunia wa Marathon mbio za Kilometa 42, Askari wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ), Sajenti Alphonce Simbu amesema anajivunia kuiheshimisha nchi yake kwa kuibuka mshindi wa Medali ya Dhahabu Jijini Tokyo, Japan hivi karibuni.
Simbu aliwasili leo saa tisa alfajiri na kupokelewa na msafara na mabasi matano huku Watumishi wenzake wa JWTZ wakiwa wamefurika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam pamoja na Bendi na Ngoma.
Mbali na Watumishi wenzake, pia Mama Mzazi wa Sajenti Simbu Salome Ntandu alishiriki mapokezi hayo pamoja na ndugu na familia yake.