Dakika ya 88 nahodha wa Wiliete anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea faulo nyota wa Yanga SC
Dakika ya 86 Yanga SC wanapata pigo huru nje kidogo ya 18 linapigwa na Ecua.
Goooooal Yanga SC
Dakika ya 82 Prince Dube anafunga goal la 3 kwa Yanga SC akiwa ndani ya 18
Dakika ya 75 mfungaji wa bao la kwanza kwa Yanga SC, Aziz anatoka nafasi yake inachukuliwa na Conte, Zimbwe Jr naye anaingia akichukua nafasi ya Boka., Duke Abuya anakuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo wa leo.
Goooooal Yanga SC
Dakika ya 72 Edmund John anafunga goal la pili kwa Yanga SC akitumia pasi ya Maxi Nzengeli
Dakika ya 70 Pacome anakwenda nje nafasi yake inachukuliwa na Celestin Ecua
Dakika ya 69 Yanga SC wanapata kona inapigwa na Pacome
Dakika ya 66 Edmund John anapewa jukumu la kupiga kona iliyosababishwa na beki wa Wiliete baada ya kuokoa krosi iliyopigwa na Boka.
Dakika ya 62 Edmund anafanya jaribio akiwa ndani ya 18 linaokolewa na mlinda mlango wa Wiliete, nyota wawili wa Wiliete ikiwa ni Daniel Nicholas wanapata maumivu kwenye harakati za kuokoa.
Dakika ya 61 Israel Mwenda anapiga krosi inakutana na Edmund John jaribio lake linaokolewa na mlinda mlango wa Wiliete.
Dakika ya 59, Maxi anaingia anatoka Mzize
Edmund John anaingia anatoka Doumbia
Dakika ya 58 Thobias anapeleka mashambulizi kwa Yanga SC, kiungo mshambuliaji wa Wiliete alifanya jaribio halikuwa na faida.
Dakika ya 55 Djigui Diarra anapeleka mashambulizi mbele na mpira unamfikia Mzize
Dakika ya 50 Wiliete SC wanafanya jaribio ambalo linakwenda nje kidogo ya 18
Dakika ya 48 Thobias anapeleka mashambulizi Yanga SC, Junior anaokoa krosi ya Mwenda na Yanga SC wanapata kona inapigwa na Doumbia inaokolewa na mlinda mlango.
Dakika ya 47 Aziz Andambwile anaanzisha mashambulizi, Doumbia anampa pasi Dube akiwa ndani ya 18 jaribio lake linaokolewa na mlinda mlango wa Wiliete SC.
Kipindi cha pili
Eddy anakwenda benchi kwa Wiliete na dakika 45 zinakwenda kuanza kutoka Angola
Mapumziko
Dakika 45 zimekamilika, Wiliete SC 0-1 Yanga SC, goal kwa Yanga SC limefungwa na Aziz Andambwile akiwa nje ya 18.
Dakika ya 45 Bacca anaokoa hatari, Mzize anapata maumivu
Dakika ya 44 Agustino anaokoa hatari na kuanzisha mashambulizi haraka kuelekea lango la Yanga SC
Dakika ya 42 Pacome anatoa krosi kwa Dube akiwa ndani ya 18 jaribio lake linaokolewa na mlinda mlango wa Wiliete.
Dakika ya 40 Yanga SC wanapata kona, kipa wa Wiliete ameokoa hatari nne ambazo zilikuwa zinakwenda kwenye lango
Dakika ya 39 nahodha wa Wiliete anatoa mpira nje inakuwa kona kwa Yanga SC, Dube anafanya jaribio kwa pigo la kichwa akitumia krosi ya Pacome inaokolewa na mlinda mlango.
Dakika ya 38 Thobias wa Wiliete anaokoa krosi iliyopigwa na Israel Mwenda
Dakika ya 37, Pacome anatoa pasi kwa Dube pembeni inaokolewa
Dakika ya 36 Wiliete wanafanya jaribio kuelekea lango la Yanga SC
Goooal Yanga
Dakika ya 31 Aziz Andambwile anafunga goal kwa Yanga SC akiwa nje ya 18 likimshinda mlinda mlango wa Wiliete SC.
Dakika ya 30 Pacome anatengeneza pasi nzuri ndani ya 18 kwa Wileiete inaokolewa na Jr
Dakika ya 28 pasi ya maelekezo kutoka kwa Doumbia inamkuta Mzize ndani ya 18, anafanya jaribio kwa mguu wake wa kushoto linakwenda nje ya 18
Dakika ya 26 Pacome anapiga krosi kuelekea ndani ya eneo la 18 kwa Wiliete SC inaokolewa
Dakika ya 25 Duke Abuya anachezewa faulo, kipa wa Wiliete SC anawapanga wachezaji wake na nyuma ya mpira yupo Pacome na Doumbia
Dakika ya 21 Prince Dube anafanya jaribio kuelekea Wiliete linaokolewa na kipa wa Wiliete SC
Dakika ya 20 Pacome anafanya jaribio ndani ya 18 linaokolewa na kipa wa Wiliete SC
Dakika ya 19 Yanga SC inapata kona inapigwa na Doumbia, Wiliete SC wanaokoa
Dakika ya 16 Duke Abuya anacheza faulo kwa mchezaji wa Wiliete SC
Dakika ya 13 Yanga SC wanatengeneza nafasi nzuri yakufunga Clement Mzize akiwa ndani ya 18 anakwama kufanya jaribio linakwenda nje ya 18
Dakika ya 12 Aziz Andambwile anampa pasi Nondo ambaye anapeleka mpira mbele , Abuya anacheza faulo kwa nyota wa Wiliete
Dakika ya 11 Agustino kipa wa Wiliete anapeleka mashambulizi mbele
Dakika ya 9 Wiliete wanapata kona ya kwanza iliyosababishwa na Boka, Diarra anaokoa pigo hilo
Dakika ya 7 Bakari Nondo anapeleka mashambulizi mbele ya Wiliete, Clement Mzize anafanya jaribio kwa pigo la kichwa linakwenda nje ya lango
Dakika ya 5 Prince Dube anafanya jaribio ambalo halileti matunda
Dakika ya 4 Clement Mzize anachezewa faulo nje kidogo ya 18
Dakika ya nne Wiliete wanarudisha mpira kwa kipa Agustino Kalougha
Dakika ya tatu Yanga SC wanapiga faulo ya kwanza kupitia kwa Doumbia
Wiliete SC 0-0 Yanga SC, mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika
Ni katika Estadio 11 de Novembro nchini Angola wakicheza na Wiliete Sports Clube.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.