SIMBA SC inapambania taji la Ngao ya Jamii mbele ya Yanga SC ambao walitwaa taji hilo msimu wa 2024/25 kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Azam FC.
Katika dakika 45 za mwanzo ubao wa Uwanja wa Mkapa unasoma Yanga SC 0-0 Simba SC ikiwa ni mchezo ambao una ushindani mkubwa ndani ya uwanja.
Beki wa Simba SC amekwama kuendelea na mchezo dakika 45 za mwanzo katika mchezo wa Kariakoo Dabi ambapo alianza kikosi cha kwanza na amefanyiwa mabadiliko nafasi yake ikichukuliwa na Chamou.
Hiki hapa kikosi cha Simba SC ambacho kimeanza dhidi ya Yanga SC:-
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.