SIMBA SC YAPATA USHINDI MBELE YA GOR MAHIA KIMATAIFA

Simba SC imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Gor Mahia kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Mkapa ikiwa ni mchezo wa kitaifa wa kimataifa.

Mabao ya Simba SC Septemba 10 2025 yamefungwa na beki wa kati Hamza Abdulrazak dakika ya 7. Ni pigo la Jean Ahoua ambaye alipiga Free Kick kwa mguu wake wa kulia ikiwa ni pasi ya goli lililofungwa na Hamza.

Goli hilo lilidumu mpaka dakika zote 45 za mwanzo kipindi cha kwanza kwa wachezaji wa Gor Mahia kukwama kuittungua Simba SC katika kilele cha Simba Day.

Steven Mukwala alifunga goli la pili dakika ya 48 akiwa ndani ya 18. Mshambuliaji huyu alitumia dakika tatu pekee kupachika bao hilo mara baada ya kipindi cha pili kuanza.

Katika kilele cha Simba Day ikiwa ni tamasha la 17 mashabiki wengi walijitokeza huku Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids akitoa ahadi kwamba msimu mpya wa 2025/25 utakuwa ni wa makombe.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.