IKIWA imebaki siku moja kabla ya tukio la Yanga Day kufanyika, kiungo mpya katika timu hiyo amejipa kazi nyingine ngumu ili awe imara zaidi.
Ikumbukwe kwamba Septemba 12, Yanga SC wamechagua kuwa na tukio la utambulisho wa wachezaji wapya na wale waliokuwa katika kikosi msimu wa 2024/25.
Offen Chikola ambaye huyu ni ingizo jipya akitokea Tabora United ameomba ruhusa kwa kocha wake Mfaransa, Romain Folz ya kutoka kambini na kwenda gmy kufanya mazoezi binafsi.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya Yanga, kiungo huyo ameomba ruhusa ya kufanya mazoezi muda wa mapumziko kwa ajili ya kujiweka sawa kuelekea msimu mpya wa 2025/26/
Haya yote yanafanyika ili kuwa na nafasi katika kikosi cha kwanza cha Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi wa ligi ya NBC ambayo inatarajiwa kuanza Septemba 17 2025.
Yanga SC kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi wanatarajia kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Bandari, Uwanja wa Mkapa.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.