YANGA SC YATAMBIA REKODI YAO, HESABU KUBWA ZINAPIGWA

UONGOZI wa Yanga SC umeweka wazi kuwa umeweka rekodi nzuri katika mashindano ya FA kwa kucheza misimu minne bila kupoteza ikiwa ni heshima na rekodi bora Afrika.

Septemba 7 2025, Yanga SC imefanya mkutano mkuu katika ukumbi wa Super Dome Masaki ambao umehudhuriwa na matawi ambayo yamekidhi vigezo na viongozi mbalimbali walikuwepo akiwemo Bi Fatma Karume ambaye ni Mjumbe wa Kudumu ndani ya Yanga SC.

Rais wa Yanga SC, Injinia Hersi Said amesema kuwa mafanikio ambayo wameyapata Yanga SC huwezi kuiweka kando juhudi za Ghalib Said Mohamed huku hesabu kubwa ikiwa ni kwenye ujenzi wa uwanja .

“Miongoni mwa rekodi kubwa ambayo tunashikilia ni kucheza misimu minne bila kupoteza kwenye Kombe la FA. Ni heshima kubwa na ya kipekee na pengine inaweza kuwa rekodi kubwa Afrika kwa sasa ninawapongeza sana wachezaji.’

“Mafanikio ya klabu hii kwa miaka ya hivi karibuni huwezi kusahau juhudi za GSM anaipenda sana klabu hii. Mara ya mwisho alituahidi kushirikiana nasi kwenye ujenzi wa uwanja. Mchakato unaendelea na dhamira bado ipo palepale. Matumaini yetu ni kufanya mambo makubwa zaidi kwa klabu hii.”

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC aliweka wazi kuwa wachezaji wamekuwa kwenye ubora mkubwa chini ya Kocha Mkuu, Romain Folz ambaye hesabu kubwa ni kupata matokeo katika mechi zote ikiwa ni pamoja na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC.

“Kocha anawapa mbinu wachezaji na jitihada zetu kuona anacheka zimekwama.Tutaanza kuona kicheko chake baada ya kutwaa taji la kwanza ambalo ni Ngao ya Jamii. Hakuna namna tupo tayari na kila kitu kinakwenda kwenye mipango makini.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.