KANUNI KWA TIMU AMBAYO HAITAFIKA UWANJANI 2025/26

WAKATI kivumbi cha Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC kikitarajiwa kuanza Septemba 17 2025, kuna maboresho ya kanuni kwa timu ambayo haitafika uwanjani bila sababu itakayokuwa inakubalika na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB)

Ni Kanuni ya 31, kutofika uwanjani inasema hivi:- Timu yoyote itakayokosa kufika uwanjani bila ya sababu za msingi zinazokubalika kwa TPLB au mchezo usifanyike itakabiliwa na adhabu ya kupoteza mchezo huo na timu pinzani itapewa ushindi wa pointi tatu na magoli matatu.

31 (1.2). Lakini pia timu kutozwa faini isiyopungua shilingi milioni hamsini (50,000,000/-) ambapo 50% ya faini itachukuliwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania na 50% italipwa kwa timu.

31 (4.1). Timu Kupokwa alama 3 katika msimamo wa Ligi pamoja na Mwenyekiti au Rais wa Klabu kufungiwa kwa kipindi cha kuanzia mwaka mmoja hadi mitano.