MERIDIANBET YAWAPA WATU WASIOONA UHURU MPYA WA KUTEMBEA

Ikiwa leo hii ni Ijumaa ya mwisho wa mwezi August, Meridianbet kama kwaida walifanya CSR kurejesha kwa jamii na safari hii walijikita kwenye kusaidia watu wenye ulemavu wa macho kwa kuwapelekea msaada wa White Cane au fimbo za kutembelea.

Kama tunavyojua kuwa binadamu tumezaliwa na changamoto mbalimbali  za kimwili basi ndivyo ambavyo walemavu wa macho nao licha ya kuwa hawawezi kuona lakini nao ni binadamu kama wengine na wanahitaji kuangaliwa kwa jicho tofauti na wengine kwani wanahitaji uangalizi zaidi.

Hivyo kwa kutambua umuhimu wao Meridianbet waliona kuwa waweze kutoa msaada angalau kidogo ambao unaweza kuwasaidia japokuwa si kumaliza tatizo lote kabisa. Kampuni hiyo kubwa ya ubashiri Tanzania waliwapelekea fimbo za kutembelea maarufu kama White Cane ambazo hizi ni muhimu kwenye maisha yao.

Leo hii tengeneza pesa kwenye michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile Poker, Keno, Roulette, Aviator, Superheli hivyo ingia na ukusanye maokoto zaidi na zaidi. PIGA *149*10# AU tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz kubashiri mechi zote.

Je unajua kuwa White Cane zina umuhimu gani kwao?. Fimbo hizi ni maalumu kabisa kwa watu wenye ulemavu ambazo hutumia kama muongozo kwao wakati wa kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Na zimetengenezwa maalumu kwaajili yao hivyo si rahisi wao kuanguka wakiwa nazo.

Meridianbet inasema kuwa msaada huu umelenga kuimarisha usalama, heshima na uhuru wa watu wenye ulemavu wa kuona, huku ukionesha dhamira ya Meridianbet katika kujali makundi maalumu ndani ya jamii. White Cane ni nyenzo muhimu inayowawezesha watu wasioona kusafiri kwa ujasiri, kufanya shughuli za kila siku kwa urahisi zaidi na kushiriki kikamilifu kwenye maisha ya kijamii na kiuchumi.

Afisa Mahusiano wa Kampuni hiyo Nancy Ingram ndiye alikuwa nahodha kwenye msafara huo ambapo baada ya kufika walipokelewa vizuri sana huku shukrani zikiwa ni kubwa sana kutoka kwa viongozi wa eneo hilo la Kindoni Manyanya.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, mwakilishi wa Meridianbet alisema: “Meridianbet tunaamini katika falsafa ya ‘Kurudisha kwa Jamii’. Leo tumegusa maisha ya ndugu zetu wenye changamoto ya kuona kwa kuwapatia fimbo za kutembelea. Tunataka waone thamani yao ndani ya jamii na waendelee kufanya shughuli zao kwa uhuru na usalama zaidi. Hii ni sehemu tu ya safari yetu ya kushirikiana na Watanzania katika kujenga jamii yenye mshikamano, upendo na fursa sawa kwa wote.”

Baada ya kupokea msaada huo kutoka Meridianbet, viongozi wa chama cha watu wasioona walitoa shukrani zao kwa mchango huu wa kipekee, wakisisitiza kuwa msaada wa aina hii ni zaidi ya kifaa cha msaada ni mwanga wa matumaini na faraja katika maisha yao, lakini pia waliwasisitiza Meridianbet kurejea tena kwa kutoa msaada wa vitu vingine ikiwemo mahitaji maalumu ya nyumbani na mengine mengi.

Meridianbet itaendelea kugusa maisha ya watu mbalimbali wenye uhitaji kwenye sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu na mengine kibao. Pia watu wengine wanahitaji kuiga mfano wa kampuni hii kubwa Tanzania kwani kutoa ni moyo si utajiri.

Mechi kibao kuendelea siku ya leo huku Meridianbet wakikwambia kuwa ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa. Unangoja nini?. Jisajili hapa na ubashiri leo.