WATATU WATAMBULISHWA YANGA SC AGOSTI, ASSINKI BEKI MGHANA NDANI

YANGA SC mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika wakiwa na mataji 31 kabatini wametambulisha nyota watatu ndani ya Agosti 2025.

Katika wachezaji hao usajili ambao ulitikisa ni ule wa beki Mohamed Hussen Zimbwe Jr aliyetambulishwa hapo akitokea kikosi cha Simba SC baada ya mkataba wake kugota mwisho msimu wa 2024/25.

Leo Agosti 21 2025 Yanga SC imtambulisha nyota mpya kuelekea msimu wa 2025/26 ambaye ni beki wa kati. Anaitwa Frank Assinki ambaye ni raia wa Ghana na msimu wa 2024/25 alikuwa ndani ya kikosi cha Singida Black Stars.

Ikumbukwe kwamba mchezaji wa kwanza kutambulishwa Agosti alikuwa ni Nahodha wa Simba SC 2024/25 Mohamed Hussen Zimbwe Jr alitambulishwa Yanga SC Agosti 6 2025 saa sita usiku.

Zimbwe Jr alitwaa tuzo ya beki bora msimu wa 2021/22. Ana tuzo ya MVP msimu wa 2016/17. Msimu wa 2023/24 alikuwa kwenye kikosi bora cha msimu ni mchezaji bora ambaye atakuwa na uzi wa Yanga SC 2025/26.

Mchezaji wa pili kutambulishwa Yanga SC ilikuwa ni Agosti 15 2025 Yanga SC ilimtambulisha rasmi winga Edmund John kutoka Singida Black Stars. Nyota huyo alitambulishwa kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Rayon Sports 1-3 Yanga SC. Kwenye mchezo huo Edmund aliazia benchi.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.